• HABARI MPYA

  Friday, February 24, 2012

  AZAM WANAJIFUA WAKIISUBIRI KWA HAMU YANGA

  MABINGWA wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC wanaendelea na mazoezi ya kujenga miili yao na mbinu ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya mechi zilizobaki za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Mazoezi yamefanyika katika uwanja wa Azam Chamazi jijini Dar es Salaam kujumuisha wachezaji wote isipokuwa wale walioitwa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'.
  Wakiwa katika mazoezi hayo beki Joseph Owino alijumuika na kikosi hicho kwa mazoezi ya kuimarisha mwili 'fitness', huku mchezaji Abdulghan Gulam akifanya mazoezi na timu ndogo kutokana na kupona jeraha la mguuni.
  Wachezaji wengine walifanya mazoezi yote mbinu na kuimarisha mwili Gym kwa muda wa masaa mawili na nusu, Gulam ataanza mazoezi na kikosi hicho kesho asubuhi.
  Akielezea umuhimu wa mazoezi hayo kocha Stewart Hall amesema kwa kipindi hiki wanatakiwa kufanya mazoezi hayo kwa kuwa hakuna mechi karibuni hivyo miili yao inatakiwa ijengeke zaidi.
  Alisema wakifanya mazoezi hiyo kwa muda wa wiki mbili watakuwa na miili imara itakayowasaidia kumalizia vyema mechi za ligi kuu zilizobaki.
  Stewart aliongeza kuwa wachezaji watafanya mazoezi ya aina hiyo kwa wiki mbili na kuendelea na mazoezi ya kawaida kwa ajili ya mechi.
  Kocha amesema siku ya Alhamis ya wiki hii atasafiri kuelekea nchini Uingereza kusalimia familia yake, wakati huo timu itakuwa chini ya kocha wa Azam Academy, Vivek Nagul akishirikiana na kocha msaidizi Kaly Ongala.
  Stewart atarejea nchini Machi 1, na kufanaya mazoezi na timu Machi 2 kabla ya kuweka kambi Maci 3 kwa ajili ya mechi dhidi ya Coastal Union itakayochezwa Machi 7 kwenye uwanja huohuo.
  Wachezaji waliohudhuria mazoezini ni golikipa Aishi Mfula, Erasto Nyoni, Abdulhalim Humud, Said Morad, Michael na Tchetche Kipre, Ibrahim Shikanda, Zahor Pazi, Hamis Mcha, Ibrahim Mwaipopo, Himid Mao, Ghulam Abdallah, na Joseph Owino.
  Jabir Aziz hakuudhuria mazoezini kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya tumbo, wachezai walioitwa timu ya taifa ni Mwadini Ally, Agrey Morris, Salum Aboubakar, John Bocco, Mrisho Ngasa Waziri Salum na Abdi Kassim.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM WANAJIFUA WAKIISUBIRI KWA HAMU YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top