• HABARI MPYA

  Friday, February 24, 2012

  CONNOR SASA KOCHA MKUU WOLVES

  KLABU ya Wolves imempandisha cheo Kocha wake Msaidizi, Terry Connor ambaye sasa atakuwa Kocha Mkuu hadi mwisho wa msimu.
  Klabu hiyo kilimfuta kazi Mick McCarthy tarehe 13 Februari mara tu baada ya kushindwa magoli 5-1 na mahasimu wao West Brom.
  Wolves wameamua kumpandisha cheo Connor baada ya Walter Smith, Alan Curbishley na Brain McDermott kuamua hawaitaki kazi hiyo ya kuiongoza Wolves.
  "Hii ni hatua muwafaka ambayo ina msimamo halisi. Wachezaji wanaiunga mkono kikamilifu", ameelezea tajiri anayemiliki klabu ya Wolves, Steve Morgan.
  "Tangu tulipofanya uamuzi kwa shida kuachana na Mick, tumepitia utaratibu kwa makini katika kumchagua mtu atakayefaa.
  "Baada ya kushauriana na watu kadha katika utaratibu huu, mimi na bodi tumeamua kwa pamoja Terry ndiye mtu atakayefaa kukiongoza klabu hadi mwisho wa msimu".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CONNOR SASA KOCHA MKUU WOLVES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top