• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 24, 2012

  PHIL NEVILLE AWA KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA VIJANA ENGLAND

  NAHODHA wa Everton, Phil Neville atajiunga na benchi la ufundi la kikosi cha timu ya taifa ya England chini ya umri wa miaka 21 kwa ajili ya mechi ya wiki ijayo, ikiwa ni hatua ya kwanza katika kujifunza ukocha.
  Beki huyo wa zamani wa kimataifa England, atapiga kazi chibni ya Brian Eastick na John Peacock kwa ajili ya mechi ya Jumatano dhidi ya Ubelgiji.
  Kocha wa England U-21, Stuart Pearce amepandishwa cheo kjuinoa timu ya wakubwa ya nchi hiyo kwa muda, akiiandaa kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Uholanzi Jumatano ijayo- baada ya Fabio Capello kujiuzulu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PHIL NEVILLE AWA KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA VIJANA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top