• HABARI MPYA

  Friday, February 24, 2012

  MASIKINI TORRES, ATEMWA HISPANIA

  KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque amemtema mshambuliaji wa Chelsea, Fernando Torres kwenye kikosi cha mabingwa hao wa Ulaya na Dunia kitakachocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Venezuela mjini Malaga Jumatano. Del Bosque amesema kutakuwa na mabadiliko kwenye kikosi kabla ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya itakayofanyika Ukraine na Poland, kwani anataka kiundwe na wachezaji ambao wamekuwa wakicheza vizuri siku za karibuni. "Ni babu kubwa, tunamkubali na inaniuma kumuacha, lakini lazima nitende haki," alisema Del Bosque kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MASIKINI TORRES, ATEMWA HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top