• HABARI MPYA

  Saturday, February 25, 2012

  SUAREZ: NDOTO ZIMETIMIA

  MSHAMBULIAJI huyo amesema alikuwa ni shabiki wa Reds wakati alipokuwa mdogo akiwa nchini kwao Uruguay na fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Cardiff City leo Jumapili ni tukio maalimu sana. Mshambuliaji huyo wa Liverpool Luis Suarez amesema kwamba “Ndoto zangu zimekuwa kweli,” kuiwakilisha klabu aliyokuwa akiipenda muda mrefu kwenye Uwanja wa Wembley,  alisema Suarez wakati Reds wako kwenye maandalizi kwa ajili ya fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Cardiff City.
  Nyota huyo wa Uruguay mwenye umri wa miaka 25, anatarajia kucheza mchezo wake wa nne kwenye michuano hiyo ya Kombe la Ligi akiwa na jezi hizo za Liverpool.
  “Kama ilivyo kwa wachezaji wengine kucheza Wembley, basin a mimi pia ndoto yangu imekamilika,” alisema Suarez.
  Suarez pia alizungumzia kufuata nyayo za akina Kevin Keegan na kocha wa sasa wa Liverpool Kenny Dalglish, ambao nao pia walivaa namba saba kama yeye, akisema ni furaha sana.
  “Wakati nakuja Liverpool sikuwa najua kama Kevin Keegan na Kenny Dalglish pia walivaa jezi namba saba lakini sasa naona ni heshima na imeongeza hamasa kwangu kuvaa jezi hii,” alisema Suarez.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SUAREZ: NDOTO ZIMETIMIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top