• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 25, 2012

  MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU ARSENAL NA SPURS KESHO


  1.                  •Msimu uliopita, Tottenham ilitoka nyuma kwa mabao mawili kipindi cha pili na kushinda 3-2, hizo zikiwa pointi tatu za kwanza kwao kuvuna kutoka Arsenal ndani ya miaka 17.

  2.                  •Msimu wa mwisho Spurs kuifunga Arsenal nyumbani na ugenini ilikuwa 1992-93), ikishinda 1-0 nyumbani na 3-1 Highbury.

  3.                  •Tangu Harry Redknapp awe kocha, Tottenham imefungwa mechi mbili tu katia ya nane ilizowakutanisha wapinzani hao wa London katika michuano yote, na moja tu katika mechi saba za Ligi Kuuwalizokutana na Gunners.

  4.                  •Tottenham imeshinda mechi moja tu katika mechi zao tano zilizopita ugenini.

  5.                  •Emmanuel Adebayor, kama atacheza, atacheza dhidi ya timu yake ya zamani katika siku ambayo atakuwa anasherehekea kutimiza miaka 28 ya kuzaliwa.

  6.                  •Chini ya Arsene Wenger, Arsenal imepoteza mechi tatu ikiwa katika mazingira ya kushinda msimu huu.

  7.                  •Lakini timu ya Mfaransa huyo imebeba pointi 10 ikiwa katika mazingira ya kupoteza, rekodi ya tatu bora katika Ligi.

  8.                  •Kwa mujibu wa Opta Sports, Theo Walcott amefanya vizuri katika krosi 14 kati ya 103 alizopiga akiwa katika nafasi nzuri msimu huu.

  9.                  •Robin van Persie amefunga mabao 21 katika mechi 20 zilizopita alizoichezea Arsenal.

  10.      •Arsenal ina wastani wa kuvuna pointi 1.7 kwa kila mechi, kiwango cha chini zaidi chini ya Wenger, wakati Tottenham ina wastani wa pointi 2.1 kwa mechi hicho kikiwa cha juu zaidi tangu Mfaransa huyo atue England.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU ARSENAL NA SPURS KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top