• HABARI MPYA

  Monday, February 20, 2012

  LIVERPOOL YAFANYA MAUAJI KOMBE LA FA, SPURS YACHELEWESHWA

  WAPIGANIA taji la Ligi Kuu ya England, Tottenham walilazimishwa sare ya bila kufungana na timu ya Daraja la Pili, katika Kombe la FA jana, wakati Liverpool na Stoke zilitinga Robo Fainali kwa matatizo.
  Spurs ilipata bao lililofungwa na Louis Saha lakini likakataliwa kwa sababu aliotea.
  Stoke— washindi wa pili wa msimu uliopita— ilipata pigo la mapema baada ya Rory Delap kupewa kadi nyekundu nab ado wakafanikiwa kuipiga timu ya Daraja la Tatu, Crawley mabao 2-0 kwa mkwaju wa penalti wa dakika ya 42 wa Jonathan Walters na bao la kichwa la dakika ya 52 la Peter Crouch.
  Liverpool inayojiandaa na fainali ya Kombe la Ligi ijayo dhidi ya Cardiff, ilishinda 6-1 dhidi ya timu nyingine ya Daraja la Kwanza, Brighton wakisaidiwa kwa mabao matatu ya kujifunga, hivyo kuungana na Sunderland, Bolton, Everton na Leicester kutinga Robo Fainali.
  Spurs ilishusha ‘muziki mzito’, bila ya Luka Modric ambaye ni majeruhi.
  Stoke, iliyofungwa 1-0 na Manchester City katika fainali ya msimu uliopita, itamenyana na Liverpool katika mechi ijayo.
  Bao la Martin Skrtel na la kujifunga la Liam Bridcutt, liliifanya Liverpool iwe mbele kwa mabao 2-1 hadi nmapumziko dhidi ya Brighton, inayofundishwa na kiungo wa zamani wa Uruguay na Chelsea, Gus Poyet.
  Bao la Andy Carroll, ambalo ni la nane msimu huu na mengine mawili ya kujifunga kipindi cha pili na lingine la Luis Suarez, ambaye pia alikosa penalti, yalikamilisha ushindi wa Liverpool.
  Everton itacheza na Sunderland, wakati mechi nyingine za Robo Fainali zitakuwa kati ya Leicester na mshindi wa mechi ya marudiano kati ya Chelsea na Birmingham ya Daraja la Kwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAFANYA MAUAJI KOMBE LA FA, SPURS YACHELEWESHWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top