• HABARI MPYA

    Tuesday, February 21, 2012

    WAMBURA AMTOA NISHAI AMIN BAKHRESA DRFA


    Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha soka (FAT) sasa (TFF), Michael Wambura amewasilisha rasmi barua ya pingamizi dhidi ya mgombea wa Uenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Amin Bakhressa.
    Wambura amesema amewasilisha barua yake DRFA na kupokelewa na mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi Kanuti Daudi alisema kwamba Katiba ya DRFA ibara ya 29 (3) inamtaka mgombea kuwa na sifa zilizoainishwa kwenye ibara ya 30(2) ya elimu ya kidato cha nne, huku ibara ya 9 ya kanuni za uchaguzi wa wanachama wa TFF inamtaka mgombea yeyoye lazima awe na elimu ya kidato cha nne inayoambatana na cheti cha matokeo.
    “Kwa mantikiti hiyo Amin Mohammed Salim (Bakhressa) anakosa sifa ya kuwa mgombea Uenyekiti wa DRFA kwa kuwa hana elimu ya kidato cha nne kinachoambatana na cheti cha matokeo, hivyo jina lake liondolewe katika orodha ya wagombea waliopitishwa kugombea uongozi wa DRFA,”Alisema Wambura.
    Aidha, Wambura pia amewatolea pingamizi wapiga kura wa DRFA Abeid Mziba (Kinondoni), Saleh Ndonga (Temeke) na Amar Balhaboo (Ilala)  ambao nao wanadaiwa kutokuwa na elimu ya kidato chga nne pamoja cheti cha matokeo.
    “Naomba kamati itamke wazi kuwa viongozi hao walichaguliwa kimakosa bila kuzingatia kanuni za uchaguzi za TFF hivyo nafasi zao zitangazwe ziko wazi  ili wapatikane watu wenye sifa za kikanuni kugombea,”Aliongeza Wambura.
    Uchanguzi wa DRFA umepangwa kufanyika Machi 18 katika sehemu ambayo itatangazwa ambapo kamatyi ya uchaguzi chini ya mwenyekiti wake Alhaj Muhidin Ndolanga imeshafanya usaili na kutanga majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAMBURA AMTOA NISHAI AMIN BAKHRESA DRFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top