• HABARI MPYA

  Monday, February 20, 2012

  MESSI AJIKUMBUSHA ALIVYOSASAMBUA ARSENAL ULAYA, APIGA NNE BARCA IKIUA 5-1 LA LIGA

  MWANASOKA bora wa dunia, Lionel Messi alitupia mabao manne nyavuni na kufikisha mabao 40 kwa msimu wa tatu mfululizo, huku akiiwezesha Barcelona kushinda 5-1 dhidi ya Valencia jana. Barcelona ilitoka nyuma na kupunguza deni la pointi hadi kubaki 10 dhidi ya vinara wa ligi hiyo, Real Madrid, ambao Jumamosi waliifunga Racing Santander 4-0.
  Muuwaji alikuwa Messi, ambaye akicheza mechi yake ya 200 ya La Liga alikutana na kipa ‘mnyela’ Diego Alves aliyemfanya afikishe mabao 27 kwenye La Liga msimu huu  na 42 kwenye mashindano yote na kwa jumla 146 katika mechi zote za ligi, akiwa na Barcelona.
  “Timu ilicheza mchezo wa kuvutia,” alisema Messi, ambaye mabao mengine manne aliyowahi kufunga katika mechi moja ilikuwa dhidi ya Arsenal kwenye Ligi ya Mabingwa miaka miwili iliyopita.
  Pablo Piatti aliifungia Valencia dakika ya tisa bao la kuongoza na Xavi Hernandez akaisawazishia Barcelona.
  Mapema, Athletic Bilbao ilifunga mabao matatu katika dakika nne za mwisho za kipindi cha pili na kuibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Malaga, wakati Levante ilipigwa 5-3 na Rayo Vallecano.
  Katika mechi nyingine ya La Liga jana, Ikechukwu Uche alipiga mabao mawili Granada ikiwafunga 4-2 Real Sociedad waliocheza pungufu ya mchezaji mmoja na Mallorca ikashinda 4-0 dhidi ya Villarreal.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MESSI AJIKUMBUSHA ALIVYOSASAMBUA ARSENAL ULAYA, APIGA NNE BARCA IKIUA 5-1 LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top