• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 25, 2012

  KILI MARATHON, ARUSHA WATAMBA KUFUNIKA 2012

  TIMU ya riadha ya Arusha imejigamba kuibuka na ushindi mnono katika mashindano ya mwaka huu ya mbio za nyika, Kilimanjaro Marathon 2012, yanayofanyika kesho mjini hapa.
  Timu hiyo ambayo imedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors ya jijini Dar es Salaam imesema mwaka huu haipo tayari kuachia medali za dhahabu, shaba na fedha ziende Kenya
  na badala yake watahakikisha kuwa zinabaki hapa nchini.
  “Tumejipanga vizuri sana mwaka huu na wachezaji wetu wote waliingia kambini kujifua vizuri chini ya udhamini mzuri wa CFAO Motors, hivyo Watanzania wake tayari kushangilia ushindi,” alisema kocha wa timu hiyo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Arusha, John Bayo.
  Aidha Bayo alisema timu ya Arusha inaundwa na wachezaji mashuhuri na walio na rekodi nzuri za mashindano hayo na yale ya kimataifa.
  Aliwataja wachezaji wanaounda timu hiyo iliyo na wakimbiaji 18 kuwa ni Fabiola William, Banuelia Katesigwa, Flora Kagali, Rebeca Kavina, Daudi Joseph, Mashaka Masumbo, Yohana
  Masuka na Josepha Elias ambao hukimbia Full Marathon.
  Wengine watakaokimbia nusu marathon (21km) ni Mary Naali, Fabian Joseph, Faustine Mussa, Ezekiel Jafari, Uwezo Lukinga, Rogart John, Joseph Francis, Restituta Joseph, Jacquline Sakilu na Damian Chopa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KILI MARATHON, ARUSHA WATAMBA KUFUNIKA 2012 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top