• HABARI MPYA

  Tuesday, February 28, 2012

  WENGER: TUNATISHA MBAYA THE GUNNERS

  KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger anasema Arsenal " bado hai " kinyume na wengi walivyofikiria baada ya kuilaza Tottenham Hotspurs kwa mabao 5-2.
  "Jinsi tulivyocheza ilikuwa safi kabisa licha ya kuanza vibaya"aliongeza.
  Bao la Louis Saha na mkwaju wa penalti wa Emmanuel Adebayor uliiweka Spurs katika hali ya kufikiria ushindi dhidi ya watani wao wa jadi.
  Lakini Bacary Sagna na Robin van Persie walisawazisha kabla ya kipindi cha mapumziko. .
  Tomas Rosicky akafunga muda mfupi baada ya kuanza kipindi cha pili na mabao mawili ya haraka yaTheo Walcott yaliwakatisha tamaa Spurs na kufufua matumaini ya Arsenal ya kufuzu kucheza katika Ligi ya Ulaya katika msimu ujao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WENGER: TUNATISHA MBAYA THE GUNNERS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top