• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 24, 2012

  STARS NA MSUMBIJI KIINGILIO BUKU TATU

  Kiingilio cha chini katika mechi ya mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Msumbiji (Mambas) itakayochezwa Februari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 3,000.
  Jumla viti 36,693 (rangi ya bluu na kijani) ndivyo vitakavyotumika kwa kiingilio hicho katika uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 wakiwa wameketi.
  Viingilio vingine ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C, sh. 15,000 kwa VIP B wakati kwa watakaokuwa miongoni mwa watakaokaa katika viti VIP A ambavyo viko 748 tu watalazimika kulipa sh. 20,000 kwa kila mmoja.
  Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Kituo cha mafuta cha Bigbon kilichopo Msimbazi (Kariakoo), mgahawa wa Steers ulioko Barabara ya Samora/Ohio, Kituo cha mafuta cha Oilcom Ubungo na Uwanja wa Taifa.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: STARS NA MSUMBIJI KIINGILIO BUKU TATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top