• HABARI MPYA

  Friday, December 07, 2018

  AZAM FC YAREJEA KILELENI LIGI KUU TANZANIA BARA BAADA YA KUICHAPA MBAO FC 4-0 LEO CHAMAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Azam FC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mbao FC usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
  Ushindi huo unaifanya Azam FC ifikishe pointi 39 baada ya kucheza mechi 15, ikiizidi kwa pointi moja Yanga SC iliyocheza mechi 14, wakati mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 27 za mechi 12 ni ya tatu.
  Katika mchezo wa leo, mabao ya Azam FC yamefungwa na beki na Nahodha, Aggrey Morris dakika ya 37, viungo Joseph Mahundi mawili dakika za 54 na 58 na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dakika ya 63.

  Azam FC ingeweza kuondoka na ushindi mnono zaidi kama ingetumia nafasi zake nyingine kadhaa ilizotengeneza kwenye mchezo huo.
  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, bao pekee la Nahodha Jacob Massawe dakika ya 38 limeipa ushindi wa 1-0 Stand United dhidi ya wenyeji, Singida United Uwanja wa Namfua, Singida.
  Kwa ushindi huo katika mchezo wake wa 16 leo, Stand United inaingia kwenye orodha ya timu tatu zenye pointi 17 pamoja na KMC iliyocheza mechi 14 na Ruvu Shooting iliyocheza mechi 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAREJEA KILELENI LIGI KUU TANZANIA BARA BAADA YA KUICHAPA MBAO FC 4-0 LEO CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top