• HABARI MPYA

  Thursday, August 09, 2018

  REAL MADRID YAMTANGAZA RASMI COURTOIS KIPA WAKE MPYA

  KLABU ya Real Madrid imethibitisha kumsajili Thibaut Courtois kutoka Chelsea kwa ada ya Pauni Milioni 35 na mkataba wa miaka sita.
  Kipa huyo atakamilisha vipimo vyake vya afya kesho na kutambulishwa makao makuu, Uwanja wa Santiago Bernabeu Saa 6:00 mchan, kabla ya kwenda kwenye mkutano na Waandishi wa Habari.
  Mateo Kovacic atahamia upande mwingine kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu mara dili la Courtois litakapokamilika.
  Taarifa ya Chelsea imesema; "Chelsea na Real Madrid usiku huu zimekubaliana vipengele vya uhamisho wa moja kwa moja wa Thibaut Courtois iwapo makubaliano binafasi yatafikiwa naye akifaulu vipimo vya afya 

  Thibaut Courtois anajiunga na Real Madrid kutokChelsea 

  "Dili hili likikamilika Mateo Kovacic atajiunga na Blues kwa mkopo wa muda mrefu,".
  Mzuia michomo hiyo wa kimataifa wa Ubelgiji amekuwa akihangaikia kuondoka Stamford Bridge kipindi chote cha majira ya joto.
  Alifikia kugoma kujiunga na timu hiyo na hakurejea kujiunga na Chelsea kwa maandalizi ya msimu mpya katika kushinikiza uhamisho wake mji mkuu wa Hispania.
  Na kwa sababu hiyo, Chelsea ikafungua taratibu za hatua za kinidhamu dhidi ya kipa huyo mwenye umri wa miaka 26 na inatarajiwa kumkata mshahara wa wiki  mbili, kiasi cha Pauni 200,000.
  Uhamisho huo unakuja baada ya Chelsea kumsajili haraka mbadala wa kipa huyo, kufuatia kukubali kumnunua mlinda mlango wa Athletic Bilbao, Kepa Arrizabalaga.
  The Blues watavunja rekodi ya dunia ya usajili wa kipa, ambayo iliwekwa na Liverpool kwa kipa Mbrazil, Alisson kwa ada ya Pauni Milioni 72 kwa kipa huyo wa kimataifa wa H.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID YAMTANGAZA RASMI COURTOIS KIPA WAKE MPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top