• HABARI MPYA

    Thursday, August 02, 2018

    MAREFA WA TANZANIA WALIOTUHUMIWA NA BURUNDI KASHFA YA RUSHWA WASAFISHWA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa majibu ya uchunguzi wa waamuzi wanne wa Tanzania waliofikishwa kwenye shirikisho hilo kufuatia kuripotiwa kwa vurugu kwenye hoteli waliyofikia nchini Burundi walipokwenda kuchezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Waamuzi waliokuwa wakichunguzwa kuhusishwa na ripoti ya mchezo huo kati ya Lydia Ludic ya Burundi na Rayon ya Rwanda ni Soud Idd Lila, Frank John Komba, Mfaume Ali Nasoro na Israel Nkongo.
    Ilidaiwa kuwa katika hoteli waliyofikia kulitokea vurugu kwa madai kuwa moja ya timu hizo mbili ilitaka kupanga matokeo kupitia waamuzi hao. 

    Frank Komba (kulia) mmoja wa marefa wa Tanzania waliosafishwa na CAF kashfa ya rushwa

    CAF katika taarifa yake iliyosainiwa na Katibu Mkuu Amr Fahmy imesema waamuzi hao wa Tanzania wako safi hakuna jambo lolote baya linalowazunguka kuhusiana na mchezo huo uliochezwa February 21,2018 Uwanja wa Prince Louis Rwagasore, Burundi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAREFA WA TANZANIA WALIOTUHUMIWA NA BURUNDI KASHFA YA RUSHWA WASAFISHWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top