• HABARI MPYA

    Tuesday, May 17, 2016

    YANGA WATUA SALAMA DUNDO TAYARI KWA KAZI NA SAGRADA ESPERANCA KESHO

    KIKOSI CHA YANGA KILICHOPO ANGOLA;
    Makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’.
    Mabeki; Juma Abdul, Mwinyi Haji, Oscar Joshua, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Pato Ngonyani na Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro'.
    Viungo; Thabani Kamusoko, Salum Telela, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke na Godfrey Mwashiuya.
    Washambuliaji; Donald Ngoma, Matheo Anthony, Amissi Tambwe na Paul Nonga.
    BENCHI LA UFUNDI;
    Kocha Mkuu; Hans van der Pluijm (Uholanzi)
    Kocha Msaidizi; Juma Mwambusi
    Kocha wa makipa; Juma Pondamali
    Daktari; Edward Bavu
    Mchua Misuli; Jacob Onyango
    Mtunza Vifaa; Mohammed Mpogolo
    Meneja; Hafidh Saleh
    WACHEZAJI WALIOBAKI DAR;
    Benedicto Tinocco, Said Juma, Issoufou Boubacar na Malimi Busungu. 


    Na Prince Akbar, DUNDO
    YANGA SC imewasili salama mjini Dundo, Angola baada ya safari ya kutwa nzima, tayari kwa mchezo wao wa kesho dhidi ya wenyeji, Sagrada Esperanca kuwania tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
    Baada ya kutua Luanda, Yanga iliunganisha ndege nyingine kwa saa mbili kwenda mji wa Dundo ambaako ni maskani ya Sagrada Esperanca.
    Yanga imefikia katika hoteli ya bora zaidi mjini humo, Diamante naa leo Saa 9:00 Alasiri kikosi chake kitashuka kwenye Uwanja wa Sagrada Esperanca mjini hapa kufanya mazoezi.
    Katika mchezo wa kesho, Yanga itahitaji sare ili kuingia hatua ya makundi, baada ya awali kushinda 2-0, mabao ya Simon Msuva na Matheo Anthony wiki iliyopita Dar es Salaam.
    Kocha Mholanzi wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema kwamba ana imani kurejea kwa wachezaji wake wawili Wazimbabwe, kiungo Thabani Kamusoko na mshambuliaji Donaldo Ngoma kutaiogezea nguvu timu yake. 
    Simon Msuva alifunga bao la kwanza katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam
    Wawili hao waliukosa mchezo wa kwanza kutokana na kuwa wanatumikia adhabu ya kadi za njano walizopewa kwenye mechi mfululizo dhidi ya Al Ahly ya Misri mwezi uliopita Dar es Salaan na Cairo, Yanga ikitolewa kwa jumla ya mabao 3-2, baada ya sare ya 1-1 nyumbani na kufungwa 2-0 ugenini.
    Mechi ya kesho itachezeshwa na marefa wa Madagascar, Hamada el Moussa Nampiandraza atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Velomanana Ferdinand Jinoro na Jean Thierry Djaonirina.
    Yanga imeangukia katika kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Shirikisho, baada ya kutolewa na Al Ahly ya Misri katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 3-2, ikilazimishwa sare ya 1-1 Dar es Salaam na kufungwa 2-1 Alexandria.
    Mwonekano wa Hoteli Diamante ambayo wamefikia Yanga SC kwa nje
    Hotel Diamanye ambayo wamefikia Yanga ina bwawa dogo la kuogelea
    Hotel Diamante ambayo wamefikia Yanga SC ina gym nzuri ya mazoezi

    Yanga ilianza vizuri tu kwa kuzitoa Cercle de Joachim ya Mauritius kwa jumla ya mabao 3-0, ikishinda 1-0 ugenini na 2-0 nyumbani kabla ya kuitoa na APR ya Rwanda kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda 2-1 Kigali na kutoa sare ya 1-1 Dar es Salaam.
    Kwa upande wao, Sagrada Esperanca katika Raundi ya Awali waliitoa Ajax Cape Town ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya kufungwa 2-1 ugenini na kushinda 2-0 nyumbani. Katika Raundi ya kwanza wakaitoa LD Maputo ya Msumbiji kwa jumla ya mabao 2-1 ikishinda 1-0 nyumbani na kutoa sare ya 1-1 ugenini na kwenda hatua ya 16 Bora, ambako waliitoa V. Club Mokanda ya Kongo kwa jumla ya mabao 4-1 wakishinda 2-1 ugenini na 2-0 nyumbani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA WATUA SALAMA DUNDO TAYARI KWA KAZI NA SAGRADA ESPERANCA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top