• HABARI MPYA

  Wednesday, May 18, 2016

  YANGA NA SAGRADA ESPERANCA KIPYENGA KUPULIZWA 'TISA JUU YA ALAMA'

  Na Prince Akbar, DUNDO
  YANGA SC inajitupa kwenye Uwanja wa Sagrada Esperanca mjini Dundo, Angola jioni ya leo kumenyana wenyeji, Sagrada Esperanca katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  Mchezo huo unatarajiwa kuanza Saa 9:00 Alasiri kwa saa za Angola na Saa 11:00 jioni kwa Saa za Tanzania.
  Yanga iliwasili Dundo usiku wa juzi baada ya safari ya kutwa nzima wakipitia Luanda, ambako waliunganisha ndege nyingine kwa saa mbili kuja mjini wa wenyeji wao, Sagrada Esperanca.
  Yanga iliyofikia katika hoteli ya bora zaidi mjini humo, Diamante, Yanga itahitaji sare ili kuingia hatua ya makundi, baada ya awali kushinda 2-0, mabao ya Simon Msuva na Matheo Anthony wiki iliyopita Dar es Salaam.
  Kila la heri Yanga SC

  Kocha Mholanzi wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema kwamba ana imani kurejea kwa wachezaji wake wawili Wazimbabwe, kiungo Thabani Kamusoko na mshambuliaji Donaldo Ngoma kutaiogezea nguvu timu yake. 
  Wawili hao waliukosa mchezo wa kwanza kutokana na kuwa wanatumikia adhabu ya kadi za njano walizopewa kwenye mechi mfululizo dhidi ya Al Ahly ya Misri mwezi uliopita Dar es Salaan na Cairo, Yanga ikitolewa kwa jumla ya mabao 3-2, baada ya sare ya 1-1 nyumbani na kufungwa 2-0 ugenini.
  Mechi hiyo itachezeshwa na marefa wa Madagascar, Hamada el Moussa Nampiandraza atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Velomanana Ferdinand Jinoro na Jean Thierry Djaonirina.
  Yanga imeangukia katika kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Shirikisho, baada ya kutolewa na Al Ahly ya Misri katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 3-2, ikilazimishwa sare ya 1-1 Dar es Salaam na kufungwa 2-1 Alexandria.
  Yanga ilianza vizuri tu kwa kuzitoa Cercle de Joachim ya Mauritius kwa jumla ya mabao 3-0, ikishinda 1-0 ugenini na 2-0 nyumbani kabla ya kuitoa na APR ya Rwanda kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda 2-1 Kigali na kutoa sare ya 1-1 Dar es Salaam.
  Kwa upande wao, Sagrada Esperanca katika Raundi ya Awali waliitoa Ajax Cape Town ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya kufungwa 2-1 ugenini na kushinda 2-0 nyumbani. Katika Raundi ya kwanza wakaitoa LD Maputo ya Msumbiji kwa jumla ya mabao 2-1 ikishinda 1-0 nyumbani na kutoa sare ya 1-1 ugenini na kwenda hatua ya 16 Bora, ambako waliitoa V. Club Mokanda ya Kongo kwa jumla ya mabao 4-1 wakishinda 2-1 ugenini na 2-0 nyumbani.
  Vikosi vya leo vinatarajiwa kuwa; Yanga; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Deus Kaseke.
  Sagrada Esperanca; Yuri Jose Tavazes, Roadro Juan da Semero, Dennis Conha Morais, Asenio Cabungula, Antonio da Silva Oliveira, Ntaku Zabakaka, Manuel Paulo Joao, Alentua Tangala Rolli, Osvaldochitumba Palana, Manuel Sallo Conha na Antonio Kasule. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA NA SAGRADA ESPERANCA KIPYENGA KUPULIZWA 'TISA JUU YA ALAMA' Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top