• HABARI MPYA

    Thursday, May 12, 2016

    WAZUNGU 'WAKABANA KOO' KUWANIA UKURUGENZI WA UFUNDI RWANDA

    MAKOCHA wanne wameingia kwenye orodha fupi ya mwisho ya kuwania Ukurugenzi wa ufundi wa Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA).
    Wanne hao ni pamoja na Mholanzi, Hendrikus Pieter de Jongh, Giovanni Scanu wa Italia, Mfaransa Sebastien Desabre na Mjerumani Michael Weiss ambao mmoja wao atachukua nafasi ya Muingereza, Lee Johnson aliyeacha kazi Aprili mwaka jana.
    “Tulipokea maombi tisa kwa ajili ya nafasi ya Mkurugenzi wa Ufundi, tukapitia maombi yao na kupata wanne wa kutathmini zaidi. Sasa tupo kwenye mchakato wa kumpata mmoja wa kuchukua nafasi hiyo, tukiwashirikisha wadau wetu wakuu, Wizara ya Michezo na Utamaduni (MINISPOC),” amesema Rais wa FERWAFA, Vincent Nzamwita.
    Rais wa FERWAFA, Vincent Nzamwita akizungumzia nafasi ya Mkurugenzi wa Ufundi

    Watano waliochujwa mapema tu ni Adalbert Ivanov Zafirov wa Bulgaria, Kiko Lopez wa Hispania, Antonio Flores Mspanyola  na Mjerumani, Drago Mamic wa Croatia na Conor Marlin wa Ireland ya Kaskazini.
    Mshambuliaji wa zamani wa Amavubi, Jimmy Mulisa atakua Mkurugenzi Msaidizi wa Ufundi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAZUNGU 'WAKABANA KOO' KUWANIA UKURUGENZI WA UFUNDI RWANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top