• HABARI MPYA

  Tuesday, May 17, 2016

  MAZEMBE YAWANG’OA WAARABU NA KUTINGA MAKUNDI

  TIMU ya TP Mazembe ya DRC imekuwa ya kwanza kwenda hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF), licha ya kufungwa mabao 2-1 jioni ya leo na wenyeji, Stade Gabesien mjini Tunis, Tunisia.
  Kwa matokeo hayo, Mazembe wanasonga mbele kwa faida ya bao la ugenini, baada ya awali kushinda 1-0 nyumbani Lubumbashi.
  Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu (pichani juu) leo aliihenyesha safu ya ulinzi ya Stade Gabesien, kabla ya kutolewa dakika ya 83 akiwa hoi kumpisha Luyindama.
  Katika mchezo wa leo, Youssef Fouzhi alianza kuwafungia wenyeji dakika ya 28 kwa penalti ya utata, kabla ya Jonathan Blingi kuisawazishia Mazembe dakika ya 70.
  Ahmed Hosni akaifungia Stade Gabesien dakika ya 75, lakini halikuisaidia timu yake kwenda hatua ya makundi.
  Kikosi cha Gabesien kilikuwa: Slim Rebai Akram Ben Sassi, Al'i Hammami, Mohamed Ben Mansour Hamza Baccouche, Aymen Kthiri Fabrice Onana/Mohamed Ben Tarcha dk60, Hamza Hadda/Wajdi Mejri dk82, Fouzhi Youssef Ahmed Hosni na Hichem Essifi.
  TP Mazembe; Gbohouo - Frimpong, Kimwaki, Coulibaly, Kasusula, Bope, Sinkala, Kalaba/Adjei dk53, Ulimwengu/Luyindama dk83, Bolingi, A na Traore/Kanda dk68.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAZEMBE YAWANG’OA WAARABU NA KUTINGA MAKUNDI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top