• HABARI MPYA

  Saturday, May 07, 2016

  KIUNGO WA CAMEROON AFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKA UWANJANI

  KIUNGO Mcameroon wa Dinamo Bucharest, Patrick Ekeng amefariki hospitali baada ya kuanguka na kupoteza fahamu uwanjani wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Romania jana.
  Cristian Pandrea, Msemaji wa hospitali ya Floreasca, amesema Madaktari walijaribu kuokoa maisha ya kijana huyo wa umri wa miaka 26, lakini wakashindwa. Sababu za kifo chake hazikujulikana.
  Dinamo ilikuwa inaongoza kwa mabao 3-2 dhidi ya Viitorul Constanta nyumbani wakati kiungo Ekeng anaanguka uwanjani dakika ya 69, zikiwa ni dakika saba tangu aingine kutokea benchi.
  Kiungo wa Dinamo Bucharest na Cameroon, Patrick Ekeng akiwa ameanguka chini baada ya kuzimia jana


  WASIFU WA PATRICK EKENG

  2008–2009: Canon Yaounde 
  2009–2013: Le Mans
  2011: Rodez (mkopo)
  2013–2014: Lausanne-Sport
  2014–2015: Cordoba 
  2016: Dinamo Bucharest
  Ekeng alianguka katikati ya uwanja na mara moja wachezaji wa timu zote wakamzunguka. 
  Taarifa ya Dinamo katika ukurasa wake wa Facebook imesema: "Dinamo usiku huu imempoteza moja kwa moja mwanasoka Claude Patrick Ekeng Ekeng,".
  "Kwa niaba ya Dinamo wote, tunawapa pole familia ya marehemu. Mungu aipumzishe kwa amani roho yake,".
  Vyombo vya habari vya Romania vimeripoti kwamba alipata na tatizo la moyo na mara moja akakimbizwa hospitali, ambako umati wa mashabiki ulikuwa nje.
  Amewahi kuchezea klabu za Cordoba ya Hispania, Lausanne ya Uswisi, na Le Mans ya Ufaransa kabla ya kutua Dinamo mwaka 2016 ambako hadi anakutwa na umauti, alikuwa amecheza mechi saba. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIUNGO WA CAMEROON AFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKA UWANJANI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top