• HABARI MPYA

    Thursday, May 19, 2016

    HAWA NDIYO WAPINZANI WA YANGA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO

    TIMU tano za Kaskazini mwa Afrika zimefuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika dhidi ya timu tatu za kanda tofauti, Mashariki, Magharibi na Afrika ya Kati.
    Timu za Kaskazini ni FUS Rabat, Kawkab Marrakech zote za Morocco, Etoil du Sahel ya Tunisia, Ahli Tripoli ya Libya na MO Bejaia ya Algeria.
    Timu hizo zinaungana na Yanga SC ya Tanzania Medeama ya Ghana na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo (DRC).
    FUS Rabat imefuzu kwa ushindi wa jumla wa 4-0, ikishinda 4-0 nyumbani dhidi ya Stade Malien ya Mali baada ya sare ya 0-0 ugenini.
    Etoile du Sahel ya Tunisia ni kati ya timu tano za Kaskazini mwa Afrika zilitonga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho

    Kawkab Marrakech imefuzu kwa ushindi wa jumla wa 2-1 dhidi ya El Merreikh ya Sudan, ikishinda 2-0 nyumbani baada ya kufungwa 1-0 ugenini.
    Ahli Tripoli imefuzu kwa bao la ugenini dhidi ya Misr Makkassa ya Misri, ikilazimisha sare ya 1-1 ugenini baada ya sare ya 0-0 nyumbani.
    Medeama imefuzu kwa bao la ugenini baada ya sare ya jumla ya 3-3 dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ikishinda 2-0 nyumbani baada ya kufungwa 3-1  ugenini.
    Etoile du Sahel imefuzu kwa ushindi wa jumla wa 2-1 dhidi ya C.F. Mounana ya Gabon ikifungwa 1-0 ugenini baada ya ushindi wa 2-0 nyumbani na Yanga SC imefuzu kwa ushindi wa jumla wa 2-1, ikifungwa 1-0 ugenini baada ya ushindi wa 2-0 nyumbani.
    TP Mazembe imefuzu kwa bao la ugenini baada ya sare ya jumla ya 2-2 dhidi ya Stade Gabesien ya Tunisia, ikifungwa 2-1 ugenini baada ya kushinda 1-0 nyumbani.
    Droo ya makundi yote, Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho inatarajiwa kupangwa Jumanne ya Mei 24, 2016 makao makuu ya CAF, Cairo nchini Misri saa 6:30 mchana.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HAWA NDIYO WAPINZANI WA YANGA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top