• HABARI MPYA

  Sunday, May 15, 2016

  HANS POPPE: TUNALETA 'MAPRO' WANNE WA KUTISHA SIMBA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  PAMOJA na mkakati wa kusajili wachezaji wanne wa kigeni wa kiwango cha juu cha juu, Simba pia imepanga kuwarudidha chipukizi wake wote iliyowatoa kwa mkopo msimu huu.
  Simba SC ilikuwa na wigo mpana wa wachezaji vijana ambao hata baada ya kuwapandisha baadhi yao, wengine hawakupata nafasi hivyo kuwatoa kwa mkopo klabu mbalimbali za Ligi Kuu.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE kwamba wamekwishaorodhesha wachezaji wa vijana waliowatoa kwa mkopo ambao sasa wameiva kuchezea timu hiyo.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema watasajili wachezaji wanne wa kigeni tishio 

  “Ni orodha ndefu, ambayo tunaendelea kuipitia taratibu na kufanya maamuzi, ila kwa sasa ambao tayari tumekwishaamua kuwarudisha ni Miraj Adam na Miraj Athumani,”amesema Hans Poppe.
  Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amesema kwamba mbali na Miraj Athumani ‘Shevchenko’ na Miraj Adam, pia kipa Dennis Richard naye anarejeshwa.
  Kuhusu wachezaji wa kigeni, Hans Poppe amesema kwamba ni mapema kuwataja.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HANS POPPE: TUNALETA 'MAPRO' WANNE WA KUTISHA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top