• HABARI MPYA

  Saturday, December 04, 2021

  TANZANITE YAICHAPA BURUNDI 3-2 KOMBE LA DUNIA


  TANZANIA imeibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Burundi jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam katika mchezo wa Raundi ya Tatu kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia kwa Wasichana chini ya umri wa miaka 20.
  Mabao ya Tanzanite leo yamefungwa na Clara Luvanga dakika ya tisa, Joyce Lema dakika ya 15 na Aisha Masaka dakika ya 44, wakati ya Burundi yamefungwa na Estella Gakima dakika ya 22 na Noella dakika ya 58.
  Timu hizo zitarudiana Desemba 18 mjini Bujumbura na mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya Botswana na Ethiopia katika Raundi ya Nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANITE YAICHAPA BURUNDI 3-2 KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top