• HABARI MPYA

  Friday, December 03, 2021

  NAMUNGO FC YAICHAPA RUVU SHOOTING 2-1 MLANDIZI


  TIMU ya Namungo FC imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
  Mabao ya Namungo FC yamefungwa na Relliant Lusajo dakika ya na Jacob Massawe dakika ya 58, wakati la Ruvu Shooting limefungwa na Rashid Juma dakika ya 46.
  Kwa ushindi huo, Namungo FC inafikisha pointi tisa na kupanda nafasi ya saba, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake tisa katika nafasi ya nane ikizidiwa wastani wa mabao na wapinzani wao wa leo baada ya wote kucheza mechi nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC YAICHAPA RUVU SHOOTING 2-1 MLANDIZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top