• HABARI MPYA

  Friday, December 03, 2021

  PRINCE DUBE AWEZA KUREJEA DHIDI YA KAGERA


  MSHAMBULIAJI Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo anaweza akarejea uwanjani Alhamisi ijayo Azam FC ikimenyana na Kagera Sugar ya Bukoba.
  Ni Azam FC ndio watakaokuwa wenyeji wa Kagera siku hiyo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Dube amekuwa nje kwa muda mrefu kutokana na maumivu na kukosekana kwake kumeipunguzia Azam FC idadi ya mabao mwanzoni mwa msimu.
  Dube amekuwa na mwendelezo mzuri mazoezini kwa wiki ya tatu sasa na baada ya mazoezi mepesi kwa muda wote, jana alianza kujifua kikamilifu na wenzake katika programu kamili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PRINCE DUBE AWEZA KUREJEA DHIDI YA KAGERA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top