• HABARI MPYA

  Friday, December 03, 2021

  MWENYEKITI AZAM MAKAMU MPYA TPLB


  MWENYEKITI wa Azam FC, Nassor Idrisa 'Father' ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) katika uchaguzi uliofanyika leo hoteli ya Cate mjini Morogoro.
  Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Jarvis Mnguto amefanikiwa kutetea nafasi yake ya Uenyekiti wa Bodi kwa awamu nyingine tena tangu ampokee kijiti aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga mwaka 2018.
  Ikumbukwe Kamati ya Uchaguzi ya TFF, chini ya Mwenyekiti, Wakili  Kiomoni Kibamba iliwaengua Mwenyekiti wa Yanga SC, Dk Mshindo Mbette Msolla na wa Simba SC, Murtaza Ally Mangungu kwa sababu tofauti.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWENYEKITI AZAM MAKAMU MPYA TPLB Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top