• HABARI MPYA

  Thursday, August 10, 2017

  AZAM FC KUCHEZA MECHI YA KWANZA ZIARA YA UGANDA LEO, WANAMENYANA NA KCCA

  RATIBA YA MECHI ZA AZAM FC
  Agosti 10, 2017; Vs KCCA
  Agosti 11, 2017; Vs Onduparaka
  Agosti 13, 2017; Vs URA 
  Agosti 14; 2017; Vs Vipers

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Azam FC leo inatarajia kukipiga dhidi ya KCCA katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika Uwanja wa Phillip Omondi, jijini Kampala, Uganda kuanzia saa 10.00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
  Azam FC ipo kwenye maandalizi makali kwenye kambi yake nchini humo kwa siku 10 ikijiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) unaoanza rasmi Agosti 26 mwaka huu.
  Kikosi cha Azam FC kiko vizuri kabisa katika kambi hiyo na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba na benchi lake zima la ufundi, wamekuwa wakifanya kazi kubwa kukipika vilivyo kikosi hicho pamoja na kuwaunganisha wachezaji kimfumo na kiuchezaji.
  Wachezaji wamekuwa wakipokea vizuri mafundisho hayo na kufurahia kiujumla kambi nzima ya hapa Uganda na wamekuwa wakionyesha ushindani mkubwa mazoezini lengo likiwa ni kila mmoja kupata namba kwenye kikosi hicho.
  Mabingwa hao wa Ngao ya Jamii na Mapinduzi Cup msimu uliopita wanaodhaminiwa na maji safi ya Uhai Drinking Water na Benki ya NMB, kabla ya mchezo huo wanatarajia kufanya mazoezi jioni ya leo kwenye uwanja huo kwa ajili ya kujiweka sawa.
  Mara baada ya mchezo huo, Azam FC inayotarajia kurejea Tanzania Agosti 15, itamalizia ziara kwa mechi nyingine tatu za kirafiki kama ifuatavyo;

  Tayari ratiba ya ligi imeshatoka, ambapo Azam FC itafunguwa pazia kwa kucheza ugenini na Ndanda katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara Agosti 26 mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC KUCHEZA MECHI YA KWANZA ZIARA YA UGANDA LEO, WANAMENYANA NA KCCA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top