• HABARI MPYA

  Thursday, August 10, 2017

  HAYATOU AMPASHA AHMAD KUTAKA KUIPORA CAMEROON AFCON 2019

  RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou juzi ‘alimuwakia’ mrithi wake, Ahmad Ahmad juu ya madai kwamba Cameroon haiko tayari kuandaa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019.
  Ahmad raia wa Madagascar, aliyehitimisha miaka 29 ya Urais wa Hayatou CAF Machi mwaka huu, amesema miundombinu ya nchi hiyo haiko tayari AFCON ya 2019 na akapendekeza kufungua maombi ya kwa nchi nyingine kuomba kuandaa fainali hizo.
  “Yeye (Ahmad) anatakiwa kwanza kuja kujionea kabla ya kuzungumza kama alivyofanya,” amesema Mcameroon Hayatou mwenye umri wa miaka 71.
  Issa Hayatou ‘amemuwakia’ mrithi wake, Ahmad Ahmad kwa kutaka kuipokonya Cameroon uenyeji AFCON 2019

  “Cameroon tayari ina viwanja vitano, bila kutaja kimoja ambacho kinaendelea kujengwa. Hakuna mtu anayeweza kusema kwamba Cameroon haijafanya chochote.Tupo ndani ya muda. Tumebakiza miaka miwili, huwezi kuuhukumu uwezo wa Cameroon AFCON miaka miwili kabla,” Hayatou.
  Ahmad amesema Kamati ya Ukaguzi wa CAF itazuru Cameroon kuanzia Agosti 20 hadi 28 kutathmini kama wanaweza kuandaa AFCON. Shirikisho la Soka Cameroon limesikitishwa na kauli ya Ahmad aliyoitoa mapema Jumatatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAYATOU AMPASHA AHMAD KUTAKA KUIPORA CAMEROON AFCON 2019 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top