MICHUANO yote ya soka Hispania itasimamishwa baadaye mwezi huu, jambo ambalo litaathiri hatua ya mwisho La Liga na fainali Copa del Rey msimu wa 2014-2015.
Mgomo huo unatarajiwa kwenye mechi za La Liga mwishoni mwa wiki ijayo kufuatia kutofikiwa makubaliano ya haki za Televisheni kwa Shirikisho la Soka Hispania kutofurahishwa na Serikali kugawana mapato.
Kwa sasa zimebaki mechi tatu kumaliza msimu wa Ligi Kuu Hispania, wakati Barcelona ikiwa inaongoza kwa pointi mbili zaidi dhidi ya Real Madrid, huku pia Barca itamenyana na Athletic Bilbao katika Fainali ya Kombe la Mfalme Mei 30.
Rasi wa Shirikisho la Soka Hispania, Angel Maria Villar ametangaza kusimamisha ligi zote
Real Madrid na Barcelona zinachuana kuwania ubingwa wa La Liga, ambayo imekumbwa na 'machafuko'
Mechi zote kuanzia Mei 16 zitasimamishwa ikiwemo fainali ya Uwanja wa Nou Camp mwishoni mwa mwezi kufuatia sheria mpya ya timu zote za madaraja mawili ya juu kugawana sawa fedha za mapato ya haki za Televisheni.
Sheria hiyo lilikubaliwa wiki iliyopita kwa lengo la kuisaidia soka ya kulipwa na pia kukuza kiwango cha mchezo huo Hispania kwa klabu za madaraja mawili ya juu kugawana fedha za haki za TV sawa.
Pamoja na hayo, wote RFEF, na Rais wake, Angel Maria Villar, na Chama cha Wachezaji (AFE) wamepinga sheria hiyo mpya na wote wamekubaliana kufanya mgomo katika soka ya Hispania.
Shirikisho linaamini sheria hiyo itavunja nguvu na pia hawaifurahii kwa sababu inakwenda kusaidia shughuli ambazo hazina umuhimu na mchezo huo.
Mashiriksiho 17 ya ya soka ya mikoa yataathirika kwa kusimamishwa ligi hiyo, wakiwemo zaidi ya wachezaji 600,000 na mechi 30,000, RFEF imesema.
Cristiano Ronaldo anaweza akawa mmoja wa waathirika wa 'machafuko' ya kisoka Hispania
Mechi za wikiendi hii zikiwemo kati ya Barcelona vs Real Sociedad na Real Madrid vs Valencia hazitaathiriwa, bali zitakazofuata zikiwemo baina ya Atletico Madrid na Barcelona Uwanja wa Vicente Calderon Mei 17.


.png)
0 comments:
Post a Comment