Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
VIGOGO wa Misri, Zamalek wamewafunga FUS Rabat ya Morocco mabao 3-2 mwishoni mwa wiki na kwenda kwenye mechi za mtoano kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Wakionekana hawana makali baada ya sare ya bila kufungana katika mchezo wa kwanza wa 16 Bora, timu hiyo ya Cairo iligeuka mbogo katika mchezo wa marudiano na kupata ushindi wa ugenini.
Mabingwa wa zamani wa Kombe la Shirikisho, FUS walianza vizuri na kufanikiwa kuongoza mabao 2-1 hadi zikiwa zimesalia dakika sita, kabla ya mabingwa mara tano wa Afrika, Zamalek kumalizia vizuri mchezo baada ya Omar Gaber kufunga bao la kusawazisha na Hazem Emam kufunga la ushindi Uwanja wa Stade du FUS.
Zamalek ni kati ya mabingwa 10 wa zamani wa Ligi ya Mabingwa walioingia kwenye mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi Kombe la Shirikisho, zikiwemo saba kutoka Kombe la Shirikisho.
AS Vita ya DRC iliwatoa Royal Leopards ya Swaziland kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya ushindi wa 4-1 jana mjini Kinshasa, ikitoka kufungwa 1-0 katika mchezo wa kwanza.
Hearts Of ya Ghana imeitoa Djoliba ya Mali kwa bao la ugenini, kufuatia ushindi wa 1-0 jana baada ya awali kufungwa 2-1 ugenini.
ASEC Mimosas imewatoa Onze Createurs kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya jana kushinda 2-0, ikitoka kushinda 1-0 ugenini mchezo wa kwanza.
Orlando Pirates imewafunga 3-0 C.F. Mounana na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-2 baada ya awali kulazimisha sare ya 2-2 ugenini.
Warri Wolves imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-1, kufuatia ushindi wa 1-0 mwishoni mwa wiki ugenini ikitoka kushinda 2-1 mchezo wa kwanza.
Etoile imeitoa Yanga SC kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya ushindi wa 1-0 mwishoni mwa wiki nyumbani, ikitoka kulazimisha sare ya 1-1 ugenini.
Club Africain imefuzu kwa ushindi wa jumla wa 2-1, baada ya kushinda 1-0 jana ikitoka kutoa sare ya 1-1 mchezo wa kwanza ugenini.
Droo ya mechi za mtoano za kuwania kucheza hatua ya makundi itafanyika kesho mjini Cairo, Misri.

![]() |
| Etoile du Sahel wamewatoa Yanga SC katika Kombe la Shirikisho |

.png)
0 comments:
Post a Comment