• HABARI MPYA

    Friday, May 08, 2015

    MALINZI ATAKA MECHI ZA MWISHO LIGI KUU ZITAZAMWE KWA JICHO LA TATU

    Malinzi (kushoto) na Katibu wake, Selestine Mwesigwa
    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewaagiza wasimamizi wa vituo vya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuhakikisha sheria na taratibu zote za mechi zinafuatwa.
    Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu huu 2014/2015 inafikia tamati kesho (Mei 9, 2015) ambapo timu zote 14 zitakuwa viwanjani katika mechi ambazo ndizo zitakazotoa hatma ya timu zinazoshuka daraja.
    Mechi hizo zitakuwa kati ya Ndanda na Yanga (Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara), JKT Ruvu na Simba (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Azam na Mgambo Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), Stand United na Ruvu Shooting (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga), Kagera Sugar na Tanzania Prisons (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Mbeya City na Polisi Morogoro (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya), na Mtibwa Sugar na Coastal Union (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI ATAKA MECHI ZA MWISHO LIGI KUU ZITAZAMWE KWA JICHO LA TATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top