// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PELLEGRINI AWAWEKEA NADHIRI CHELSEA, ASEMA LAZIMA AWACHINJE JANUARI 31 DARAJANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PELLEGRINI AWAWEKEA NADHIRI CHELSEA, ASEMA LAZIMA AWACHINJE JANUARI 31 DARAJANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, January 19, 2015

    PELLEGRINI AWAWEKEA NADHIRI CHELSEA, ASEMA LAZIMA AWACHINJE JANUARI 31 DARAJANI

    KOCHA wa Manchester City, Manuel Pellegrini amesema kwamba kipigo jana kimewapunguza spidi katika mbio za kutetea uabingwa wa Ligi Kuu ya England na sasa wanalazimika kuwafunga wapinzani wao katika mbio hizo, Manchester City Uwanja wa Stamford Bridge ili kufufua matumaini.
    City ililala 2-0 mbele ya Arsenal jana Uwanja wa Etihad mabao ya Santi Cazorla kwa penalti dakika ya 24 na Olivier Giroud la pili kwa kichwa dakika ya 67.
    Kipigo hicho kinamaanisha timu ya Pellegrini inazidiwa pointi tano na Chelsea, ambayo juzi iliifunga Swansea 5-0, Sasa washindano hao wa ubingwa wa England msimu huu watakutanana Stamford Bridge Januari 31.
    Manuel Pellegrini looks up to the heavens in despair during Manchester City's 2-0 defeat by Arsenal

    "Mchezo ujao tunaokwenda kucheza Stamford Bridge ni muhimu sana. Lazima tupunguze idadi ya pointi tunazozidiwa (na Chelsea) hadi kubaki mbili. Natumai tutazunduka na kucheza na mchezo wetu,"amesema Pellegrini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PELLEGRINI AWAWEKEA NADHIRI CHELSEA, ASEMA LAZIMA AWACHINJE JANUARI 31 DARAJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top