• HABARI MPYA

  Tuesday, January 06, 2015

  MAN UNITED YAPEWA TENA VIBONDE RAUNDI YA NNE KOMBE LA FA

  TIMU ya Manchester United imepangiwa tena mpinzani kibonde, wa Daraja la Pili katika Raundi ya nne ya Kombe la FA, Cambridge United. 
  Kikosi cha Louis van Gaal kitasafiri hadi Uwanja wa Abbey mwishoni mwa January wakati Mholanzi huyo akipambana na kukata kiu ya miaka 11 ya United kutottwaa Kombe la FA. 
  Mashetani hao Wekundu walifuzu wamefuzu hatua hiyo baada ya kuifunga 2-0 timu ya Daraja la Kwanza, Yeovil Town katika Raundi ya Tatu.  
  Angel di Maria and his Manchester United team-mate will face League Two outfit Cambridge United 
  Angel di Maria na wachezaji wenzake wa Manchester United watamenyana na timu ya Daraja la Pili, Cambridge United 

  RATIBA RAUNDI YA NNE KOMBE LA 

  Southampton/Ipswich vs Crystal Palace
  Cambridge vs Manchester United
  Blackburn vs Swansea
  Chelsea vs Millwall/Bradford
  Derby vs Scunthorpe/Chesterfield
  Preston vs Sheffield United
  Birmingham City vs West Brom
  Aston Villa vs Bournemouth
  Cardiff vs Reading
  Liverpool vs Bolton
  Burnley/Tottenham vs Leicester
  Brighton vs Arsenal
  Rochdale vs Stoke
  Sunderland vs Fulham/Wolves
  Doncaster/Bristol City vs Everton/West Ham
  Manchester City vs Middlesbrough
  Mechi zitachezwa wikiendi ya Januari 24 na 25 mwaka 2015
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAPEWA TENA VIBONDE RAUNDI YA NNE KOMBE LA FA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top