• HABARI MPYA

  Monday, January 05, 2015

  DAN SSERUNKUMA AWAPA ‘NENO’ SIMBA SC

  Na Mahmoud Zubeiry, ZANZIBAR
  MSHAMBULIAJI wa Simba SC, Mganda Dan Sserunkuma amewaomba mashabiki wa timu hiyo wampe muda ili azoee hali na kuanza kufanya vitu vyake.
  Sserunkuma aliyesajiliwa kutoka Gor Mahia ya Kenya, ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba kama ataendelea kupangwa na kuendelea kuzoea muda si mrefu ataanza kuwafurahisha wapenzi wa Simba SC.
  “Najua watu wa Simba walitarajia mambo makubwa haraka sana kutoka kwangu. Lakini wasikate tamaa, mpira si jambo rahisi kama wengi wanavyofikiria,”.
  Dan Sserunkuma ameomba wana Simba SC wampe muda

  “Kutoka klabu nyingine, nchi nyingine, ligi nyingine ambayo iko tofauti na nchi uliyohamia, klabu uliyojiunga nayo na Ligi unayokwenda kucheza inahitaji muda kumudu mabadiliko,”amesema.
  Sserunkuma amesema hana wasiwasi kabisa kwamba atafanya vizuri katika klabu yake mpya, lakini kwanza apewe muda ili azoee.
  Tayari Sserunkuma amekwishacheza mechi nne na kufunga mabao mawili, yote katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Taifa Jang’ombe kwenye ushindi wa 3-1 Zanzibar.
  Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes amehamia kwenye Ligi ya Tanzania baada ya kung’ara katika Ligi ya Kenya kwa misimu mitatu, akiibuka mfungaji bora wa ligi hiyo mara mbili mfululizo na sasa anatarajiwa kuhamishia mafanikio yake hayo Msimbazi.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DAN SSERUNKUMA AWAPA ‘NENO’ SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top