Wednesday, November 05, 2014

    MKUDE: SIJASAINI SIMBA SC, NATAKA MILIONI 80 KWANZA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KIUNGO Jonas Mkude amesema kwamba hajasaini Mkataba mpya na Simba SC na anataka Sh. Milioni 80 ili kufanya hivyo, iwe kwa klabu yake hiyo, au nyingine yoyote itakayojimudu kutoa dau hilo.
    Hata hivyo, akizungumza na BIN ZUBEIRY leo, Mkude amesema kwamba anatoa kipaumbele kwa klabu yake, Simba SC katika hilo iwapo watakuwa tayari kumpa Milioni 80 za Tanzania.
    “Sijasaini Mkataba mpya na Simba SC. Kwa sasa naelekeza nguvu zangu kwenye mechi na Ruvu Shooting (Jumapili), baada ya hapo nitafungua milango ya mazungumzo ya Mkataba mpya,”amesema.
    Jonas Mkude amesema anataka Sh. Milioni 80 kusaini Mkataba mpya

    Mkude amesema kwamba amebakiza miezi sita katika Mkataba wake wa sasa na Simba SC, hivyo ni wakati mwafaka kwake kuanza kuzungumzia Mkataba mpya.
    Mkude alipandishwa kikosi cha kwanza cha Simba SC mwaka 2011 akitokea timu ya vijana ya klabu hiyo na tangu kifo cha kiungo Patrick Mafisango yeye ndiye ameziba pengo hilo katika nafasi ya kiungo wa ulinzi.
    Kwa sasa, Mkude ni mchezaji kipenzi cha wapenzi wa Simba kutokana na juhudi zake na kujituma awapo uwanjani.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MKUDE: SIJASAINI SIMBA SC, NATAKA MILIONI 80 KWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry