• HABARI MPYA

    Wednesday, October 08, 2014

    SHEREHE ZA MIAKA 50 YA TFF FIFA, MARAIS WOTE TANZANIA, BAKHRESA NA STARS YA 1980 LAGOS KUPEWA TUZO

    Na Mwandihi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) leo (Oktoba 8 mwaka huu) linaadhimisha miaka 50 ya kujiunga na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
    Katika kuadhimisha siku hii, TFF ilipanga kufanya tafrija fupi ya kuwaenzi wale wote waliotoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania katika kipindi hicho cha miaka 50.
    Hafla hii itafanyika katika siku nyingine itakayopangwa.
    Katika hafla hiyo, TFF itatoa tuzo kwa watu na taasisi mbalimbali zilizochangia maendeleo ya michezo ka miaka yote hiyo, wakiwemo Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere (marehemu), Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya KIkwete.
    Mwenyekiti wa Makampuni ya S.S.B. Limited, Alhaj Sheikh Said Salim Bakhresa

    TFF pia itakabidhi tuzo kwa makampuni wadhamini, Said Salim Bakhresa Group Limited, TBL, Vodacom (T) Ltd, SBL, NMB, AIRTEL, Bank ABC Ltd, Coca Cola (T) Ltd, NSSF, Africa Barrick Gold, Air Tanzania Ltd, TRC, Symbion Power Ltd, Bodi ya Tumbaku, Bodi ya Pamba, Bodi ya Kahawa, BIMA, Geita Gold Mine, 
    Mtibwa Sugar Estate Limited, Kagera Sugar Limited na Tanga Cement.
    Wachezaji waliokuwemo kwenye kikosi cha Taifa Stars kati ya mwaka 1979 1980, ambacho kilishiriki Fainali za Mataifa ya Afrika nchini Nigeria pia watatuzwa kwenye hafla hiyo.
    KIkosi hicho chini ya Nahodha, Leodegar Tenga wengine ni Athumani Mambosasa, Idd Pazi, Juma Pondamali, Leopold Mukebezi, Ahmed Amasha 
    Mohamed Kajole, Salim Amir, Jella Mtagwa, Mtemi Ramadhan, Adolf Rishard, Hussein Ngulungu, Juma Mkambi, Omari Hussein, Thuweni Ally, Mohamed Salim, Peter Tino, Rashid Chama, Slomir Wolk (Kocha Mkuu), Joel Bendera (Kocha Msaidizi), Dk. Katala (Daktari wa timu), Mzee Mwinyi (Meneja  wa timu), Willy Kiango, Daud Salum na Stanford Nkondora (Mkuu wa Msafara).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SHEREHE ZA MIAKA 50 YA TFF FIFA, MARAIS WOTE TANZANIA, BAKHRESA NA STARS YA 1980 LAGOS KUPEWA TUZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top