MASHABIKI wa Manchester United wanaoendesha kampeni ya ‘Njoo Nyumbani Ronaldo’ wanaonekana kuanza kufanikiwa mapema katakana na Cristiano Ronaldo kuwa na ratiba ya kurejea Old Trafford mapema mwezi ujao.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Chama cha Soka Argentina vimesema kutakuwa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa baina ya Argentina na Ureno uliopangwa kufanyika Novemba 18.
Mchezo huo utawapa nafasi nyingine ya 'dhahabu' mashabiki wa United kumshawishi mshambuliaji huyo wa Real Madrid arejee Old Trafford.
Cristiano Ronaldo na Lionel Messi kulia watakutana katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Old Trafford mwezi ujao
0 comments:
Post a Comment