• HABARI MPYA

    Tuesday, October 07, 2014

    DI MATTEO KOCHA MPYA SCHALKE ITAKAYOMENYANA NA CHELSEA LIGI YA MABINGWA NOVEMBA 25

    MTALIANO Roberto Di Matteo ameteuliwa kuwa kocha mpya wa Schalke baada ya klabu hiyo ya Bundesligakumfuta kazi Jens Keller kufuatia mwanzo maimu huu.
    Mwanasoka huyo wa zamani wa kimataifa wa Italia, ambaye aliiwezesha Chelsea kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa kocha mwaka 2012, amekuwa hana timu tangu afukuzwe na klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England Novemba mwaka huo. 
    Di Matteo, ambaye alirithi mikoba Rafa Benitez Stamford Bridge, aliendelea kulipwa mshahara wake wa Pauni 130,000 kwa wiki The Blues hadi Juni mwaka 2014. Schalke itamenyana na Chelsea 25 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

    Di Matteo aliendelea kulipwa Pauni 130,000 kwa wiki hadi Juni 2014 na Chelsea
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DI MATTEO KOCHA MPYA SCHALKE ITAKAYOMENYANA NA CHELSEA LIGI YA MABINGWA NOVEMBA 25 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top