• HABARI MPYA

    Saturday, June 07, 2014

    KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2014; KUNDI A LENYE BRAZIL, CAMEROON WATATOKA?

    WENYEJI wa Kombe la Dunia wapo kundi moja na Mexico, Croatia na Cameroon.
    Hapa, BIN ZUBEIRY inakuletea makala ya mchambuzi na beki wa zamani wa England, Martin Keown juu ya mtazamo wake katika Kundi Group A.

    Mcheza kwao hutuzwa: Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia, Brazil 
    Kundi A
    Brazil
    Croatia
    Mexico
    Cameroon
    Utabiri wa Keown;
    1 Brazil
    2 Mexico
    3 Cameroon
    4 Croatia
    Ratiba (Saa za Afrika Mashariki)
    Jun 12        Brazil v Croatia            Saa 5:00 usiku  S. Paulo 
    Jun 13
            Mexico v Cameroon    Saa 1:00 usiku  Natal 
    Jun 17 
           Brazil v Mexico            Saa 4:00 usiku  Fortaleza 
    Jun 18
            Cameroon v Coatia     Saa 7:00 usiku  Manaus 
    Jun 23 
           Croatia v Mexico         Saa 5:00 usiku  Recife 
    Jun 23
            Cameroon v Brazil       Saa 5:00 usiku  Brasilia 
    BRAZIL
    Viwango vya FIFA: Namba 3
    Kocha: Luiz Felipe Scolari. Anarejea kwa mara ya pili kuifundisha Brazil baada ya kuipa Kombe la Dunia mwaka 2002.
    Nahodha: Thiago Silva (PSG)
    Mchezaji wa kumlikwa: Neymar (Barcelona) Katika Kombe la Mabara nilimuona akipiga mipira ya adhabu mazoezini. Alifanya vizuri. Alifunga mara tank mfululizo. Ana kipaji na nafasi ya kuwa gwiji wa Brazil.
    Ubora wao: Si kwa sababu ni timu ya Wabrazil. Scolari ameiunganisha timu nzuri kucheza soka maridadi ya ushindi.
    Hatari: Si sana. Tatizo kubwa litakuwa kukabiliana na presha.
    Watakwenda England? Sehemu kubwa ya wachezaji katika kikosi chao wanatoka Ligi Kuu ya England, lakini pia nyota wa Bayern Munich, Dante na Luiz Gustavo wa Wolfsburg wanatakiwa na Arsenal na klabu nyingine.
    Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Washindi (1958, 1962, 1970, 1994 na 2002)
    Je, wajua? Brazil wameshinda fainali tano kati ya saba walizotinga.
    In the spotlight: Young superstar Neymar is the one to watch as Brazil look to win for the sixth time
    Wa kumulikwa: Nyota kinda, Neymar ni mchezaji wa kutazamwa Brazil ikiwania taji la sita la Kombe la Dunia
    CROATIA  
    Viwango vya FIFA: Namba 18
    Kocha: Niko Kovac. Mara ya kwanza ukocha wa timu kubwa, baada ya kuiongoza U21 ya Croatia.
    Nahodha: Darijo Srna (Shakhtar Donetsk) 
    Mchezaji wa kumulikwa: Mateo Kovacic (Inter Milan). Anajituma sana anapocheza ndani, lakini pia hushambulia anapohitajika.
    Ubora wao: Ina mabeki wa pembeni wanaoshambulia sana. Nahodha Srna amekuwa akishambulia kutokea beki ya kulia kwa miaka kadhaa sasa.
    Check him out: Mateo Kovacic will be looking to pull the strings for Croatia in Group A
    Mtu wa kumulikwa: Mateo Kovacic anatarajiwa kuiongoza Croatia kutoka Kundi A

    Hatari: Hawana safu imara ya kiungo na hilo jambo ambalo kocha wao anatakiwa kulifanyia kazi usiku na mchana.
    Atakwenda England? Mshambuliaji Mario Mandzukic yupo kwenye orodha ya wachezaji wanaotakiwa Arsenal sambamba na Chelsea na Manchester United.
    Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Washindi wa tatu (1998)
    Je, wajua? Wimbo halisi wa taifa wa Croatia awali ulikuwa una urefu wa vesi 14. Bahati, ni vest ya kwanza, ya pili, 13 na 14 pekee ndizo zitakazoimbwa katika Kombe la Dunia.
    MEXICO   
    Viwango vya FIFA: Namba 20
    Kocha: Miguel Herrera. 
    Nahodha: Rafael Marquez (Leon)
    Mchezaji wa kumulikwa: Oribe Peralta (America) mfungaji wao bora katika mechi za kufuzu na ambaye kwa sasa amekuwa mchezaji ghali katika soka ya Mexico aliyeuzwa kwa Pauni Milioni 6.
    Ubora wao: Kutoka kwenye kundi. Mexico imefuzu kuinfia hatua ya mtoano katika Fainali tank zilizopita za Kombe la Dunia.
    Leader: Rafael Marquez is the Mexico captain
    Kiongozi: Rafael Marquez ni Nahodha wa Mexico

    Hatari: Hawana msimamo. Mexico imetumia wachezaji 47 na makocha wanne tofauti wakati wa mechi za kufuzu.
    Watakwenda England? Liverpool inamfuatilia kipa Guillermo Ochoa wa Ajaccio na beki wa kati, Hector Moreno wa Espanyol ni shabiki mkubwa wa Everton na Swansea.
    Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Kufika Robo Fainali (1970 na 1986)
    Je, wajua?: Miguel Herrera alikataa kuchukua wachezaji wanaocheza Ulaya katika mechi ya mchujo ya kufuzu dhidi ya New Zealand. Alisema hawatamudu umbali wa safari. 
    CAMEROON   
    Viwango vya FIFA: Namba 56 
    Kocha: Volker Finke. Ameiongoza Freiburg kwa miaka 16.
    Nahodha: Samuel Eto'o (Chelsea)
    Mchezaji wa kumulikwa: Vincent Aboubakar (Lorient) Macho yore yataelekezwa mshambuliaji pacha wake, Eto'o, lakini kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa na msimu mzuri Ufaransa, akifunga mabao 11 katika mechi 21.
    He knows where the goal is: Striker Samuel Eto'o (left) will lead the line for Cameroon in Brazil
    Anafahamu lilipo lango: Mshambuliaji Samuel Eto'o (kushoto) ataiongoza Cameroon nchini Brazil

    Ubora wao: Bado wagumu. Wamefanya uteuzi mzuri wa viungo wakabaji na wameruhusu mabao manne tu katika mechi nane za kufuzu. 
    Hatari: Eto'o ni mshambuliaji mzuri na mzoefu, lakini wana tatizo katika safu ya kiungo, ambalo wamejaribu kulitafutia ufumbuzi kwa kumuandaa Alex Song kuichezesha timu.
    Watakwenda England? Kiungo wa zamani wa Arsenal, Song amepewa ofa ya kurejea Ligi Kuu ya England, wakati beki wa Marseille, Nicolas Nkoulou anafuatilia na Arsenal na Newcastle kwa karibu.
    Matokeo mazuri Komb la Dunia: Kufika Robo Fainali (1990) 
    Je, wajua?: Katika Fainali za Italia mwaka 1990, Cameroon iliweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kabisa kuongoza kundi ikiwa haina bao baada ya kutoa mabao ya kufunga na kufungwa (GD 0).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2014; KUNDI A LENYE BRAZIL, CAMEROON WATATOKA? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top