KIUNGO tegemeo wa Ujerumani, Marco Reus yuko hatihati kukosa Fainali za Kombe la Dunia baada ya kutonesha kifundo chake cha mguu akiichezea nchi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Armenia ikishinda 6-1.
Kiungo huyo alitolewa dakika ya 43 timu yake ikiwa haijapata bao hats moja na kipindi cha pili ikatikisa nyavunza wapinzani mara sita.
Reus alipelekwa hospital kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi na taarifa zaidi inatarajiwa kutolewa leo juu ya hali yake na mustakabali wake kwenye michuano hiyo inyoanza baadaye mwezi huu Brazil.
0 comments:
Post a Comment