MABINGWA watetezi wa Kombe la Dunia, Hispania wapo kundi moja na Chile, Australia na washindi wa pili wa mwaka 2010, Uholanzi.
BIN ZUBEIRY inaendelea kukuketea makala za mchambuzi na beki wa zamani wa England, Martin Keown hapa akilichamua Kundi B.
Kundi B
Hispania
Uholanzi
Chile
Australia
Utabiri wa Keown;
1 Uholanzi
2 Hispania
3 Chile
4 Australia
Ratiba (Saa za Afrika Mashariki)
Jun 13 Hipania v Uholanzi Saa 4:00 usiku Salvador
Jun 13 Chile v Australia Saa 7:00 usiku Cuiaba
Jun 18 Australia v Uholanzi Saa 1:00 usiku P. Alegre
Jun 18 Hispania v Chile Saa 4:00 usiku R. Janeiro
Jun 23 Australia v Hispania Saa 1:00 usiku Curitiba
Jun 23 Uholanzi v Chile Saa 1:00 usiku Sao Paulo
Jun 13 Chile v Australia Saa 7:00 usiku Cuiaba
Jun 18 Australia v Uholanzi Saa 1:00 usiku P. Alegre
Jun 18 Hispania v Chile Saa 4:00 usiku R. Janeiro
Jun 23 Australia v Hispania Saa 1:00 usiku Curitiba
Jun 23 Uholanzi v Chile Saa 1:00 usiku Sao Paulo
HISPANIA
Viwango vya FIFA: Namba 1
Kocha: Vicente del Bosque. Kutwaa mfululizo Kombe la Dunia yatakuwa mafanikio makubwa.
Nahodha: Iker Casillas (Real Madrid)
Mchezaji wa kumulikwa: Sergio Ramos (Real Madrid). Staili ya uchezaji ya viungo wa Hispania imekuwa kivutio, lakini mwishoni mea msimu Ramos alikuwa babu kubwa. Anaweza kumkabili mshambuliaji peyote na usomaji wake wa mchezaji umemfanya we bora na bora.
Wanakwenda tena: Beki wa Hispaia, Sergio Ramos akiwaq ameinua Kombe la Dunia miaka mine iliyopita
Ubora wao: Kukaa na mpira, hakuna ubishi kwamba linapokuja suala la kumiliki mpira, Hispania wanatisha- wanakaa na mpira 'siku nzima.
Hatari: Mabao yamepungua. Mwaka uliopita wameweza kufunga zaidi ya mabao mawili katika mechi mbili tu.
Watakwenda England? Diego Costa yuko njiani kutua Chelsea wakati Cesc Fabregas anaweza kuungana naye earajani.
Matokeo mazuri Kombe la dunia: Washindi (2010)
Walivyofika hapa: Waliongoza kundi lao kwa rekodi ya kutopoteza mechi kati ya nane walizocheza, wakishinda sita na kutoa sare mbili.
Je, wajua?: Mara ya mwisho nyavu za Hispania kuguswa katika hatua ya mtoano kwenye mashindano makubwa ilikuwa kwenye 16 bora ya Kombe la Dunia mwaka 2006.
UHOLANZI
Viwango vya FIFA: Namba 15
Kocha: Louis van Gaal. Anakabiliwa na mtihani wa kuiongoza Uholanzi, wakati huo huo kufikiria namna ya kuisuka upya Man United.
Nahodha: Robin van Persie (Manchester United)
Tegemeo la Uholanzi: Robin van Persie ana matumaini Uholanzi itafanya vizuri mwaka huu Kombe la Dunia zaidi ya miaka minne iliyopita
Mchezaji wa kumulikwa: Daley Blind (Ajax). Mtoto wa shujaa wa zamani wa Uholanzi, Danny, ni mtaalamu haswa. Ameisaidia Ajax kushinda Ligi Kuu, akihamishwa kutoka kucheza beki ya kushoto hadi kiungo.
Ubora wao: Kutumia nafasi. Uholanzi imefunga mabao 34 katika mechi zao 10 za kufuzu.
Hatari: Kumalizia mashindano. Uholanzi walifungwa kwa mara ya tatu wakifika fainali Kombe la Dunia mwaka 2010, rekodi ambayo sasa wanaishikilia wao na Ujerumani.
Watakwenda England? Daley Blind, Daryl Janmaat, Bruno Martins Indi wametajwa Manchester United, Everton na Arsenal; Swansea wanampenda Jordy Clasie wakati Memphis Depay anavutiwa pia.
Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Washindi wa pili (1974, 1978 na 2010)
Walivyofika hapa: Waliongoza kibabe kundi lao wakishinda mechi tisa kati ya 10 walizocheza.
Je, wajua? Hii ni mara ya pili Van Gaal anaiongoza timu hiyo ya taifa. Mara ya kwanza haikufuzu Kombe la Dunbia 2002 alipokuwa nayo.
CHILE
Viwango vya FIFA: Namba 14
Kocha: Jorge Sampaoli. Muargentian aliyevuka mpaka hadi kutua Chile, anayetarajiwa kutamba na staili yake ya uvaaji kofia ya baseball.
Nahodha: Claudio Bravo (Real Sociedad)
Mchezaji wa kumulikwa: Alexis Sanchez (FC Barcelona). Ni mtu hatari kweli, ambaye alikuwa sababu ya England kufungwa na Chile Novemba mwaka jana. Anacheza pembeni ya Lionel Messi kwa Barcelona, lakini ni tegemeo kubwa la Chile katika safu ya ushambuliaji.
Sura maarufu: Wachezaji wa Hispania wanamjua vizuri mshambuliaji wa Chile anayechezea Barcelona, Alexis Sanchez
Ubora wao: Wanacheza kwa kasi na kujituma. Sampaoli anatumia mfumo sawa na wa Marcelo Bielsa aliyeiongoza timu hiyo mwaka 2010 wakati walipokuwa moja ya timu zilizoburudisha kwa soka maridadi kwenye michuano hiyo.
Hatari: Kukosa Mwendelezo. Walishinda mechi tisa za kufuzu, sawa na Argentina, lakini wakafungwa sita, mbili na Argentina.
Watakwenda England? Gary Medel ataondoka Cardiff lakini anaweza kurudi Hispania, Hull inampenda Jean Beausejour wakati United, Liverpool na Arsenal wote wanaweza kumtaka Sanchez iwapo dau watalimudu.
Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Mshindi wa 3 (1962)
Walivyofika hapa: Walimaliza nafasi ya tatu kwenye kundi nyuma ya Argentina na Colombia, wakishinda mechi tisa kati ya 16, na kutoa sare moja tu.
Je, wajua? Chile haijawahi kufika Fainali ya Kombe la Dunia, lakini walishika nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia la U20 na U17 sambamba na Michezo ya Olimpiki
AUSTRALIA
Viwango vya FIFA: Namba 62
Kocha: Ange Postecoglou. Muaustralian mzaliwa wa Ugiriki ana uzoefu na Kombe la Dunia– akiwa amewahi kuziongoza timu za vijana za U17 na U20 kwenye michuano hiyo ya FIFA.
Nahodha: Mile Jedinak (Crystal Palace).
Mchezaji wa kumulikwa: Matthew Ryan (FC Bruges). Kustaafu kwa Mark Schwarzer ni pigo kwenye lango la Australia, lakini mzuia michomo huyo kinda anaweza kuwa mrithi wake wa kudumu.
Ubora wao: Mashambulizi yao ya nguvu ya krosi kutoka pembezoni mwa Uwanja yanatisha huku Tim Cahill akitegemewa kumalizia.
Hatari: Safu ya ulinzi shaka tupu. Kustaafu kwa wachezaji wake wazoefu kumepunguza uimara wa safu ya ulinzi ya Australia.
Watakwenda England? Hakuna mengi ya kuandika juu ya Jedinak, lakini Tommy Oar mwenye umri wa miaka 22, wing anayechezea FC Utrecht nchini Uholanzi ndiye pekee ambaye klabu zinamfuatilia.
Matokeo mazuri Kombe la Dunia: 16 Bora (2006)
Walivyofika hapa: Walishika nafasi ya pili katika kundi la Asia kufuzu Kombe la Dunia, wakizidiwa pointi nne na vinara Japan.
Je, wajua? Tim Cahill hive karibuni alipewa heshima ya kipekee baada ya barabara mjini Sydney kupewa jina lake ‘Tim Cahill Expressway’.



.png)
0 comments:
Post a Comment