• HABARI MPYA

    Friday, June 06, 2014

    GEBO PETER KUZIKWA KESHO KIGURUNYEMBE

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam Gabriel Peter Magali, maarufu kama Gebo Peter atazikwa kesho kijijini kwao, Kigurunyembe mkoani Morogoro.
    Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa taarifa ya kuupokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji mrefu, aliyekuwa mkali wa kufunga mabao ya vichwa enzi zake.
    Gebo ambaye pia kama kaka yake Agustino Peter ‘Peter Tino’  alichezea timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ameaga dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) mjini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
    Marehemu Gebo enzi za uhai wake

    Gebo aliyezaliwa mwaka 1961, pia aliwahi kuchezea timu za Sigara ya Dar es Salaam, CDA ya Dodoma na kombaini ya Mkoa wa Dar es Salaam (Mzizima United). Hadi mauti yanamkuta alikuwa akijishughulisha na biashara, kubwa ikiwa ya vifaa vya michezo.
    Kwa sasa, msiba upo nyumbani kwao Vingunguti karibu na Kanisa Katoliki, Dar es Salaam ambapo taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na familia.
    Marehemu ambaye ameacha mjane na watoto watatu. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GEBO PETER KUZIKWA KESHO KIGURUNYEMBE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top