• HABARI MPYA

    Tuesday, September 03, 2013

    LUKAKU ATUA EVERTON KWA MKOPO

    IMEWEKWA SEPTEMBA 3, 2003 SAA 10:30 ALFAJIRI
    kLABU ya Everton imeshinda vita dhidi ya West Brom kuwania saini ya mshambuliaji wa Chelsea, Romelu Lukaku kwa mkopo wa muda mrefu.
    Kiungo wa kimataifa wa England, Gareth Barry pia ametua Goodison Park kwa msimu mmoja akitokea Manchester City. 
    Lukaku alitarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha Jose Mourinho msimu huu, lakini kuwasili kwa Samuel Eto'o kama mchezaji huru amepoteza uhakika wa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
    Romelu Lukaku
    Haikuwa bahati yake: Nyota wa Ubelgiji alitarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha Chelsea msimu huu

    Roberto Martinez amefanikiwa kuinasa saini ya mchezaji huyo licha ya kukata tamaa na pamoja na kutakiwa pia na West Brom ambako mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20alicheza kwa mkopo msimu uliopita- akifunga mabao 17 katika Ligi Kuu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: LUKAKU ATUA EVERTON KWA MKOPO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top