IMEWEKWA SEPTEMBA 3, 2013 SAA 9:50 USIKU
KLABU ya Manchester United imemsaini Marouane Fellaini kutoka Everton kwa Pauni Milioni 27.5.


Kupitia Sportsmail, BIN ZUBEIRY inafahamu David Moyes ameungana na kijana wake wa zamani baada ya kumfukuzia kwa muda mrefu, akibebwa na maombi yake ya mapema kwa mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ubelgij.
Mwishowe United wamekata kiu kwa kumpata mchezaji waliyekuwa wakimtaka, ingawa wamelipa Pauni Milioni 3.5 zaidi kutoka walizotoa kumnunua Robin van Persie msimu uliopita.
Ameondoka: Marouane Fellaini anatua Manchester United
Kiungo huyo wa Ubelgiji, Fellaini amekuwa akitakiwa kuungana na kocha wake wa zamani, Moyes na hakuwa na chaguo zaidi, isipokuwa kutua United.
Fellaini amepewa ruhusa ya kuchelewa kujiunga na kikosi chake cha timu yake ya taifa, ili kukamilisha uhamisho wake mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kutua United, ambao ulikuwa unashughulikiwa na baba yake, Abdellatif.
United ilituma ofa tofauti kwa wote Fellaini na Leighton Baines mapema majira haya ya joto, ikianza na Pauni Milioni 28 jumla kwa wote na baadaye Milioni 36, ambazo zote zilipigwa chini na Everton.
Na inafahamika kwamba United ilijaribu kumsajili Mesut Ozil aliyetua Arsenal kwa Pauni Milioni 42 kutoka Real Madrid na ilitoa ofa iliyodunda na Pauni Milioni 34 kwa mchezaji mwingine wa Real, Sami Khedira kabla ya kujaribu kwa nyota wengine wa klabu hiyo Luka Modric bila mafanikio.
Wameungana tena:Kocha wa Manchester United, David Moyes alifanya kazi na Fellaini alipokuwa Everton
walengwa: Wote Fellaini (kushoto) na Leighton Baines (kulia) waliichezea Everton huko Cardiff Jumamosi


.png)