IMEWEKWA MEI 15, 2013 SAA 2:25 USIKU
KLABU ya Malaga ya Hispania imesema kocha wake, Manuel Pellegrini yuko huru kuhamia Manchester City ya England.
Kwa mujibu wa taarifa nchini Hispania, raia huyo wa Chile amekubali mkataba wa miaka miwili kwenda Etihad kurithi mikoba ya Mtaliano Roberto Mancini, aliyefukuzwa usiku wa Jumatatu.
City sasa itafanya taratibu rasmi za kumuomba Pellegrini, ingawa kocha huyo Malaga hakuwa pekee anayetakiwa kuziba nafasi ya Mancini, kwani hata Jose Mourinho wa Real Madrid anatajwa pia.
Nichague mimi: Manuel Pellegrini amekubali mkataba wa miaka miwili kupiga kazi Man City. Kulia ni Jose Mourinho anayetajwa pia kuwa na nafasi ya kumrithi Mancini.