• HABARI MPYA

    Wednesday, May 15, 2013

    CHELSEA NA ARSENAL KUCHEZA MECHI MAALUM KUSAKA MSHINDI WA TATU LIGI KUU ENGLAND

    IMEWEKWA MEI 15, 2013 SAA 6: 30 MCHANA
    KLABU za Arsenal na Chelsea zinaweza zikamaliza Ligi Kuu ya England zikiwa zinalingana kwa kila kitu, pointi na wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa hivyo kulazimika kucheza mechi maalum baina yao kutafuta timu ya kushika nafasi ya tatu.
    Ushindi wa 4-1 wa Arsenal 4-1 dhidi ya Wigan unamaanisha The Gunners wamefikisha pointi 70 na wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa 34, huku ikiwa imefunga mabao 71 msimu huu. 
    Heading for fourth: Lukas Podolski celebrates after scoring against Wigan
    Wamezinduka: Lukas Podolski akishangilia kufunga dhidi ya Wigan
    Record breaker: Chelsea's Frank Lampard helps his side move up to third
    Mvunja rekodi: Kiungo wa Chelsea, Frank Lampard ameisaidia timu yake kupaa nafasi ya tatu

    Hii inamaanisha ikiwa Chelsea itatoka sare ya bila mabao na Everton Uwanja wa Stamford Bridge katika mechi ya mwisho na kikosi cha Arsene Wenger kikaifunga Newcastle kwa wastani wa bao moja, iwe 2-1, 3-2, 4-3, timu hizo zitalingana kwa kitu.
    Kwa kuwa nafasi ya tatu inaifanya timu ifuzu moja kwa moja kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa badala ya kuanzia kwenye kuwania kufuzu, inamaanisha kushika nafasi ya tatu ni hatua nzuri.
    BIN ZUBEIRY kupitia Sportsmail inatambua kwamba Ligi Kuu England imekwishaanza kuandaa mechi hiyo maalum iwapo itatokea. 
    Uwezekano wa kumaliza msimu kwa mechi maalum ulipangwa zamani, rejea msimu wa 1995-96 wakati Manchester United na Newcastle United zilipokuwa zinagombea ubingwa. 
    Licha ya mchuano mkali wa jino kwa jino, mwisho wa siku United ilishinda mbio za ubingwa bila mechi maalum.
    Inafahamika kama kutakuwa na mchezo huo maalum, basi utafanyika mara moja tu msimu utakapomalizika na kwa vyovyote utachezwa London.
    Rule

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: CHELSEA NA ARSENAL KUCHEZA MECHI MAALUM KUSAKA MSHINDI WA TATU LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top