• HABARI MPYA

  Ijumaa, Mei 31, 2013

  KOCHA TIMU YA TAIFA ITALIA AJA JUU BALOTELLI KUHUSISHWA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA, AONYA; "MUMKOME"

  IMEWEKWA MEI 31, 2013 SAA 2:00 USIKU
  MUMKOME Balotelli. Huo ndio ujumbe wa kocha wa timu ya taifa ya Italia, Cesare Prandelli siku moja baada ya mshambuliaji huyo kuhusishwa na kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kundi la wahalifu la Neopolitan Camorra. 
  Akizungumza na TV ya taifa ya Italia leo, kuelekea mchezo wa kirafiki dhidi ya San Marino, Prandelli alisema: "Haivumiliki kuendelea kumfuatafuata na kumuhusisha na kila kitu,"alisema.
  Milan man: Mario Balotelli with his girlfriend Fanny Neguesha out shopping
  Mtu wa Milan: Mario Balotelli akiwa na mpenzi wake Fanny Neguesha kwa ajili ya shopping
  On international duty: Balotelli training with Italy
  Majukumu ya kimataifa: Balotelli akifanya mazoezi na timu ya taifa ya Italia

  Tuhuma ziliibuka wakati wa kutoa ushahidi katika kesi ya fedha haramu, ambayo Balotelli pia alitoa ushahidi mwaka 2011 kuhusu kuwatembelea jirani zake wa Scampia wanaohusishwa na uhalifu mapema huo.
  Balotelli amekasirika kuhusishwa na biashara hiyo na amesema hahusiki , wakati Prandelli amemalizia kwa kusema: "Siwezi hata kufikiria yeye kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya kama utani,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: KOCHA TIMU YA TAIFA ITALIA AJA JUU BALOTELLI KUHUSISHWA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA, AONYA; "MUMKOME" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top