• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 28, 2013

  BENITEZ KOCHA MPYA NAPOLI KWA MIAKA MIWILI


  IMEWEKWA MEI 28, 2013 SAA 10:45 ALFAJIRI
  ALIYEKUWA kocha wa muda wa Chelsea, Rafa Benitez ametangazwa rasmi kuwa kocha mpya wa Napoli kwa mkataba wa miaka miwili.
  Mspanyola huyo mwenye umri wa miaka 53 alikutana na Rais wa klabu hiyo, Aurelio de Laurentiis Jijini London ambaye alithibitisha kwenye ukurasa wake wa Twitter: "Rafa Benitez sasa ni kocha mpya wa Napoli. Mtu mwenye uzoefu mkubwa wa kimataifa. Kiongozi,".
  Mtayarishaji huyo wa filamu, De Laurentiis dili ilikuwa likamilishwe tangu Ijumaa iliyopita, lakini walilazimika kufanya subira, ili kwanza Benitez akamilishe majukumu yake Chelsea.
  Benitez aliyeikuta Chelsea katika hali mbaya baada ya kufukuzwa kwa Mtaliano Roberto Di Mateo anaiacha vizuri timu na Kombe la Europa League sambamba na nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.
  Chelsea sasa inarudi mikononi mwa kocha wake wa zamani na kipenzi cha mashabiki wa Stamford Bridge, Mreno, Jose Mournho anayeondoka Real Madrid. 
  Deal: Rafa Benitez shaking hands with Napoli president Aurelio de Laurentiis
  Mpango mzima: Rafa Benitez akipeana mikono na Rais wa Napoli, Aurelio de Laurentiis
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: BENITEZ KOCHA MPYA NAPOLI KWA MIAKA MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top