• HABARI MPYA

  Ijumaa, Mei 24, 2013

  CHELSEA YATAKA KUSAJILI BONGE LA WINGA LA ATLETICO MADRID


  IMEWEKWA MEI 24, 2013 SAA 12:00 ASUBUHI
  KLABU ya Chelsea imeonyesha nia ya kumsajili winga wa kimataifa wa Uturuki, Arda Turan, ambaye kwa sasa anachezea Atletico Madrid. 
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, ameivutia klabu yake ya zamani, Galatasaray lakini rais wake, Unai Aysal amesema wanakabiliwa na upinzani kutoka Stamford Bridge.
  Centre of attention: Chelsea have truned their attention to Atletico Madrid's Arda Turan
  Katikati ni kivutio: Chelsea imeonyesha nia ya kumsajili nyota wa Atletico Madrid, Arda Turan

  Alisema: "Chelsea wamo kwenye mbio za kumsajili Arda na hatutakuwa tayari kushindana na ofa watakayotoa. 
  "Nimekutana na kiongozi wa Atletico Madrid, ameniambia kwamba kulikuwa kuna wachezaji watatu hawataki kuwauza, mmoja wao ni Arda Turan.'
  Centre of attention: Chelsea have truned their attention to Atletico Madrid's Arda Turan
  Wakati huo huo, Atletico ni miongoni mwa klabu ambazo zinammezea mate kiungo wa QPR, Esteban Granero. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, pia anatakiwa na Fulham, Sevilla na Real Betis. 
  Na Manchester City iko tayari kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wa Hispania, Dennis Suarez kwenda Sevilla, Granada na Espanyol wanaomuhitaji mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: CHELSEA YATAKA KUSAJILI BONGE LA WINGA LA ATLETICO MADRID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top