• HABARI MPYA

  Jumapili, Mei 26, 2013

  BINTI WA GEWE NDIYE MISS UKONGA 2013

  Miss Ukonga 2013 katika picha ya pamoja na washindi wake wa pili na wa tatu

  Na Princess Asia, IMEWEKWA MEI 26, 2013 SAA 2:31 USIKU
  KAZI inazidi kuwa pevu katika safari ya kumsaka Redd’s Miss Tanzania 2013, baada ya warembo wengine kupatikana katika mchakato wa awali wa kuelekea safari ya kumpata yule atakayevikwa taji hilo.
  Kazi kubwa ilikuwa ni pale Redds Miss IFM na Redd’s Miss Ukonga walipokuwa wanasakwa juzi, huku kukiwa na ushindani mkali kutoka kwa warembop waliokuwa wakiwania taji hilo.
  Shindano la Redd’s Miss IFM lililoleta ushindani mkubwa katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dar es Salaam ilishuhudia Jesca Nasari akiondoka na taji hilo.
  Jesca alikabidhiwa taji hilo na mshindi aliyepita ambaye alikuwa ni Fina Revocatus, huku nafasi ya pili ikitwaliwa na Miriam Manyanga na Shamimy Mohammed.
  Redd’s Miss IFM, Jesca ataungana na washindi hao wengine katika kukiwakilisha chuo hicho katika shindano la Redd’s Miss High Learning litakalofanyika mwishoni mwa mwezi ujao. Mrembo huyo pia alikabidhiwa Sh milioni 1 taslimu kama zawadi ya ushindi.
  Katika Ukumbi wa Wenge Garden uliopo Ukonga Mombasa, Dar es Salaam kulikuwa na kinyang’anyiro kingine cha kumsaka Redd’s Miss Ukonga.
  Katika shindano hilo Martha Gewe alifanikiwa kutwaa taji hilo na hivyo kuchukua nafasi ya Elizabeth Pretty aliyemaliza muda wake.
  Mratibu wa shindano hilo, Chiku Chambuso alitoa angalizo kwa warembo wengine na kusema kwa sasa Ukonga imepania kufanya kweli zaidi na wanaamini watamtoa Redd’s Miss Tanzania.
  Kinyang’anyiro cha vitongoji mbalimbali ikiwa ni safari ya kuelekea Redd’s Miss Tanzania kinatarajiwa pia kuendelea mwishoni mwa wiki.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: BINTI WA GEWE NDIYE MISS UKONGA 2013 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top